Uganda:kutangaza injili ni zawadi ya kushirikishana! - | vatican news

Vaticannews

Uganda:kutangaza injili ni zawadi ya kushirikishana! - | vatican news"

Play all audios:

Loading...

Kutangaza Injili ni zawadi ya kishirikshana.Kama wakristo,wafuasi wa Yesu,mtindo wetu wa maisha lazima uangazie imani yetu,tujiulize kwa kina sisi ni nani na kwa nini tunaishi.Hatuko peke


yetu.Kristo ni msikilizaji wa kimya kwa kila uongofu na anabisha hodi katika mioyo yetu kwa kusubiri aweze kufunguliwa ili aingie na kuishi.Ni maneno ya Padre Kaweesa Mkurugenzi wa PMS


katika kukaribisha mwezi wa Kimisionari. Katika harakati za maandalizi ya Mwezi wa Kimisionari ulimwenguni, Oktoba 2020, Padre Pontian Kaweesa, Mkurugenzi wa Shughuli za Kipapa za


Kimisionari (PMS) nchini Uganda amezungumzia juu ya maandalizi yanayofanywa na Kanisa mahalia kwamba: “Kutangaza Injili ni zawadi ya kishirikshana”. “Kama wakristo, wafuasi wa Yesu, mtindo


wetu wa maisha lazima uangazie imani yetu, tujiulize kwa kina sisi ni nani na kwa nini tunaishi. Hatuko peke yetu. Kristo ni msikilizaji wa kimya kwa kila uongofu na anabisha hodi katika


mioyo yetu kwa kusubiri aweze kufunguliwa ili aingie na kuishi nasi”, amesema Padre Kaweesa. SHUGHULI ZA KIPAPA ZA KIMISIONARI (PMS) NCHINI UGANDA ZINASINDIKIZA WAAMINI KUISHI NA KUKUA KAMA


NDUGU, KAKA NA DADA AMBAO LAZIMA waendelee kujua wema, huruma na upendo wa Mungu. Wiki iliyopita anaripoti Padre Pontian kuwa serikali ya Uganda imefungua shughuli za kiliturujia ambazo


baada ya miezi saba hivi ilikuwa imekatazwa mikusanyiko ya Ibada kutokana na Janga la COVID-19. Idadi ya waamii washiriki kwa kila adhimisho la Misa hawapaswi kuzidi watu 70. Kwa mujibu wa  


Mkurugenzi wa kitaifa wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari( PMS) amesema, “tumewahamasisha wabatizwa wote kusali pamoja katika familia zao na hivyo Kanisa kuendelea na kazi yake ya


uinjlilishaji wa familia. NENO LA MUNGU LIMETANGAZWA NA MAKATEKISTA, NA WAAMINI WALEI WANAOTIMIZA WAJIBU WAO VYEMA NA MAKASISI AMBAO WAMEENDELEA KUwatembelea familia na Jumuiya ndogondogo za


kikristo na kuwahudumia kwa kuwapatia sakramenti za ubatizo, Ekaristi Takatifu na Ndoa Takatifu. Kwa kujivunia  katika umoja na Baba Mtakatifu, Padre Kaweesa amesema, wamevuka salama


kipindi hiki cha janga la Corona huku wakiwasaidia wagonjwa na jamii zilizoathirika. Madhara makubwa yaliyoletwa na janga hili ni kuharibika kwa uchumi huku familia nyingi zikikosa uwezo wa


kujikimu kimatibabu. HATA HIVYO, KWA UFAFANUZI ZAIDI AMESEMA KUWA HUDUMA NYINGI ZIMEWEZA KUTOLEWA NA WAAMINI WA KANISA KATOLIKI WA UGANDA NA PIA WAKIBUNI mbinu mbalimbali za kuandaa siku ya


kimisionari duniani mwaka 2020. Padre Pontian vile vile ameelezea kwamba wameandaa mikakati inayowasilisha utume wa kimisionari wa Kanisa zima na Kanisa mahalia utakaotangazwa kwa njia ya


televisheni ya kikatoliki Uganda (UC TV) na matangazo mbashara kupitia Radio Maria ili kuzungumzia utume wa kimisionari katika nyakati hizi za janga la COVD-19.   KWA UPANDE WA HABARI ZA


KIMATAIFA, WAMEWAOMBA MAASKOFU KURIDHIA PENDEKEZO LA KUFUNGUA AKAUNTI AMBAPO WAAMINI WATAWEKEZA fedha na mbinu nyingine za kifedha. Wakurugenzi wa PMS wamewaandikia Maaskofu wa Majimbo (POM)


ili kuwaomba waamini waendelee kuombea umisionari wa Kanisa na kufanya Novena kabla ya maadhimisho ya siku ya Misioni duniani wakiongozwa na kauli mbiu “tazama mimi hapa nitume” (Is 6:8)


iliyosambazwa katika mitandao. “sasa ni wakati wa kuipeleka Injili mbele” amehitimisha Padre Kaweesa huku akisisitiza kuwa kila zawadi ni vema ikashirikishwa kwa wengine.


Trending News

404 - ukurasa haujapatikana

Nenda kwenye maudhuiNenda kwenye orodha kuuNenda tovuti zaidi za DWVidio zetuSauti zetuMaeneoTanzaniaKenyaJamhuri ya Kid...

Macron kujadili wimbi la ghasia za kisiwa cha caledonia

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anafanya kikao na mawaziri waandamizi mchana huu kujadili wimbi la ghasia linaloshuhudi...

Pentekoste:sala ya malkia wa mbingu katika uwanja wa mtakatifu petro! - | vatican news

Tarehe 31 Mei 2020 ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Ujio wa Roho Mtakatifu,Papa Francisko ataadhimisha Misa ka...

Trump aifutia kibali cha mafuta venezuela

Akitangaza uamuzi huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social siku ya Jumatano (Februari 26), Rais Donald Trump ...

Urusi – DW

Nenda kwenye maudhuiNenda kwenye orodha kuuNenda tovuti zaidi za DWVidio zetuSauti zetuMaeneoTanzaniaKenyaJamhuri ya Kid...

Latests News

Iran yaanza kuhesabu kura, wahafidhina wakitarajiwa kushinda

Uchaguzi huo wa jana Ijumaa ndiyo ulikuwa wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliosababishwa na kifo cha mwanamke wa Kik...

Sweden kuimarisha doria za mpakani

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ülf Kristensen, amewaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi kuhusiana na suala hilo utatolewa...

404 - ukurasa haujapatikana

Nenda kwenye maudhuiNenda kwenye orodha kuuNenda tovuti zaidi za DWVidio zetuSauti zetuMaeneoTanzaniaKenyaJamhuri ya Kid...

Uganda:kutangaza injili ni zawadi ya kushirikishana! - | vatican news

Kutangaza Injili ni zawadi ya kishirikshana.Kama wakristo,wafuasi wa Yesu,mtindo wetu wa maisha lazima uangazie imani ye...

Papa francisko: hija ya kichungaji: marche! Tetemeko la ardhi! - | vatican news

Papa Francisko anatarajiwa kutembelea Jimbo kuu la Camerino-Sanseverino, nchini Italia. Haya ni maeneo yaliyoathirika sa...

Top