Israel,hali ya kibinadamu huko Gaza ni ya kukata tamaa.Maelfu ya watu wana njaa

Vaticannews

Israel,hali ya kibinadamu huko Gaza ni ya kukata tamaa.Maelfu ya watu wana njaa"

Play all audios:

Loading...

Vita Nchi za Mashariki kati ya Israel na Palestina:vifo vingi kila siku.  (ANSA) Ulimwengu Israel,hali ya kibinadamu huko Gaza ni ya kukata tamaa.Maelfu ya watu wana njaa 30 Oktoba 2023


baada ya mapumziko ya saa chache,urushaji wa maroketi kutoka Gaza kuelekea jamii za Waisrael walio karibu na Ukanda huo,hasa mji wa Netivot,ulianza tena.Kuna idadi ya watu wenye njaa


waliozingirwa,wakati huo idadi ya vifo imeongezeka hadi 8 elfu.Gutterres:hali inakatisha tamaa. Na Angella Rwezaula, - Vatican.


Malori 30 ya misaada ya kibinadamu tayari yamewasili Gaza, na 24 ya mwisho katika masaa machache yaliopita, japokuwa hayatoshi kutuliza njaa ya wakazi wa Ukanda uliozingirwa kila kona.


Kulingana na wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu, usaidizi bado haufai kitu kwa  mahitaji baada ya maelfu ya watu kuvamia maghala ya Umoja wa Mataifa kutafuta chakula. Katika


mazungumzo ya simu kati ya  Rais wa Marekani Joe Biden alimtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuongeza mtiririko wa mahitaji muhimu kwa ajili ya  raia. Na wakati idadi ya wahanga


wa Kipalestina, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, imefikia 8,000, hali hiyo inaning'inia kwa uchungu juu ya mateka 239 wa Israel ambao bado wako mikononi mwa Hamas, ambao kuachiliwa kwao


hakuna mazungumzo madhubuti ambayo bado yameanza.


Shambulio kali dhidi ya Hamas Wakati huo huo, jeshi la Israel linaendelea kuzidisha mashambulizi dhidi ya Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza: wakati wa usiku, kulingana na kile


kilichotangazwa na msemaji wa kijeshi,  kuwa  walishambulia “magaidi kadhaa ambao walikuwa wamejizuia katika majengo na vichuguu, wakijaribu kushambulia Wanajeshi wa Israel. Mashambulio ya


Israel pia dhidi ya Siria na Lebanon. Mapigano pia yalitokea katika Ukingo wa Magharibi, na Wapalestina 4 waliuawa na 9 kujeruhiwa huko Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi. Kwa hiyo


baada ya kusimama kwa saa chache, urushaji wa roketi kutoka Gaza kuelekea jamii za Israeli karibu na Ukanda huo, hasa mji wa Netivot, pia ulianza tena. Wakati huo huo, polisi walitangaza


kuwa wametambua miili ya Waisraeli 1,135 waliouawa tangu kuanza kwa shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7: na  823 ni raia na askari 312. Hotuba ya Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa


la Kuhudumia Wakimbizi, Filippo Grandi, inatarajiwa tarehe 30 Oktoba 2023 katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


Gutterres hali inakuwa ya kukatisha tamaa kila saa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameanza ziara yake rasmi nchini Nepal kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za


wanafunzi 10 wa Nepal waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas nchini Israel, na kwa mara nyingine tena kutoa wito wa kulindwa kwa raia wote huko Gaza na kwamba: “hali


inakuwa ya kukatisha tamaa kila saa.”  Ziara ya Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa inakuja wakati mgogoro katika Ukanda wa Gaza ukiingia Juma la  tatu kufuatia uvamizi uliofanywa mnamo tarehe 7


Oktoba 2023 na wapiganaji wa Hamas ndani ya Israel na baadae Israel kutangaza vita. Kwa mujibu wa  taarifa kutoka Umoja wa Mataifa unabainisha kuwa Mwishoni mwa Juma lililopita (27 Oktoba


2023)Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano kwasababu za kibinadamu, lakini siku chache zilizopita kumeshuhudiwa mashambulizi makubwa ya mabomu na ripoti


za operesheni za ardhini zinazofanywa na Israel ndani ya Gaza. Kwa njia hiyo akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pushpa Kamal Dahal, Mkuu wa Umoja wa mataifa katika mkutano na waandishi


wa habari Dominika tarehe 29 Oktoba 2023 alisema: “Ninajua kwamba ingawa mzozo wa Mashariki ya Kati uko umbali wa maelfu ya kilomita umepiga karibu sana na nyumbani kwa watu wa Nepal.” 


Hakuna uhalali wowote kwa mauaji na kujeru wala kuteka nyara Na akitoa salamu za heri za kurejea salama kwa Bipin Joshi, raia wa Nepal ambaye ametoweka na aliapa ataendelea kusisitiza


kuachiliwa huru mara moja na bila masharti kwa mateka wote huko Gaza alisema: Na ninarudia kulaani kwangu kabisa mashambulizi ya kutisha yanayofanywa na Hamas. Hakuna uhalali wowote, kwa


mauaji, kujeruhi na kutekwa nyara kwa raia,”. Wakati huo huo, Bwana Guterres alibainisha hali mbaya sana ya Gaza na kueleza masikitiko yake kwamba badala ya kustekelezwa kwa sitisho muhimu


kwa sababu za kibinadamu azimio lililoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, Israel imezidisha operesheni zake za kijeshi. “Idadi ya raia ambao wameuawa na kujeruhiwa haikubaliki kabisa. Pande


zote lazima ziheshimu wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu ... ambayo iliibuka kutokana na janga na uzoefu mbaya wa vita."  Akisisitiza wito wake thabiti wa kufuata


kikamilifu sheria za kimataifa za kibinadamu, Katibu Mkuu alisema: “Sheria za Vita huweka sheria wazi za kulinda maisha ya binadamu na kuheshimu masuala ya kibinadamu. Sheria hizo haziwezi


kubadilishwa kwa ajili ya manufaa.”


Lazima tuunganishe nguvu kukomesha jinamizi hili Bwana Guterres alisema kuwa huko Gaza zaidi ya watu milioni mbili wasio na mahali popote salama pa kwenda, wananyimwa mahitaji muhimu ya


maisha - chakula, maji, malazi na matibabu - huku wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara. “Ninawasihi wale wote walio na wajibu kuondoka kutoka ukingoni," alisema akiitaja hali hiyo


kama “janga la kibinadamu.” Katibu Mkuu alisisitiza ombi lake la kusitishwa kwa mapigano mara moja kwa sababu za kibinadamu, kuachiliwa huru bila masharti kwa mateka wote, na utoaji wa


misaada endelevu ya kibinadamu kwa kiwango ambacho kinakidhi mahitaji ya watu wa Gaza. “Lazima tuunganishe nguvu ili kukomesha jinamizi hili kwa watu wa Gaza, Israel na wale wote


walioathirika duniani kote, ikiwa ni pamoja na hapa Nepal,” alisema.


Kujitolea kwa Nepal kwenye ushirikiano wa kimataifa na SDGs Katibu Mkuu amesifu utamaduni wa muda mrefu wa nchi hiyo iliyoko Himalaya kwa kutetea amani na ushirikiano wa pande nyingi na


kuitaka dunia “kuwa rafiki bora wa Nepal”, ambayo imekumbwa na machafuko ambayo haijajiletei yenyewe, ikiwa ni pamoja na tishio la machafuko yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Bwana Gutterres alimshukuru Waziri Mkuu Dahal na kusema kwamba Umoja wa Mataifa unaishukuru sana Nepal kwa uungaji mkono wake kwa masuluhisho ya pande nyingi – pamoja na kuwa iliunga mkono


mchango wake mkubwa katika misheni za kulinda amani duniani kote. Mwanzoni mwa ziara yake ya siku nne nchini humo, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia alisifu "maendeleo ya kustaajabisha” ya


Nepal katika miongo miwili iliyopita, kwani imekuwa jamhuri, imeanzisha amani, na kujidhatiti kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu(SDGs) na hatua za kukabiliana na mabadiliko


ya tabianchi.


 'Kuhitimu' kunakaribia “Na kuna mengi zaidi yajayo, Bwana Guterres aliendelea, akielezea kwamba miaka michache ijayo itakuwa ya maamuzi, wakati Nepal inajiandaa kuhitimu kutoka hadhi ya


Nchi Zenye maendeleo duni. Katibu Mkuu alikuwa akizungumzia mchakato unaowezeshwa na Umoja wa Mataifa ambapo mataifa yaliyo hatarini zaidi duniani yakishakidhi vigezo (juu ya kipato, mali ya


binadamu na udhaifu wa kiuchumi na kimazingira), yanaweza kuchukua hatua za kuelekea 'kuhitimu' inawakilisha hatua muhimu katika njia ya maendeleo ya LDCs. Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa


aliendelea kubainisha kuwa katika miaka michache Ijayo, Nepal pia itaanza hatua za mwisho za mchakato wa amani: mpito wa kuelekea kwenye haki. "Mpito kuelekea kwenye haki lazima usaidie


kuleta amani kwa waathiriwa, familia na jamii," alisema, akisisitiza kwamba "Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono Nepal kuandaa mchakato unaokidhi viwango vya kimataifa, maamuzi ya


Mahakama ya Juu, na mahitaji ya waathirika - na kuyatekeleza kwa vitendo.” Umoja wa Falme za Kiarabu unaliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) ambalo linakutana Jumatatu 30


Oktoba 2023 kwa ajili ya azimio la lazima la "kusitishwa mara moja ghasia huko kwa ajili ubinadamu huko Gaza". Rasimu ya azimio inayozunguka inazungumzia "kusitishwa mara moja kwa ajili ya


ubinadamu" na zaidi "hofu ya kibinadamu".


Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba. 30 Oktoba 2023, 11:30 Tuma Chapa


Trending News

Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 17:Wajumbe wanapendekeza marekebisho ya hati ya mwisho

Vatican Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 17:Wajumbe wanapendekeza marekebisho ya hati ya mwisho Katika mkutano wa waandishi w...

Idhaa ya kiswahili 16. 09. 2023 - | vatican news

__ The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the serv...

Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 16 Septemba 2018 - | Vatican News

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Bwana awe nanyi ! Awe rohoni mwa...

Kipindi cha majilio: jiandaeni vyema kukutana na kristo yesu! - | vatican news

Jumapili ya kwanza ya kipindi cha Majilio inaufungua rasmi Mwaka Mpya wa Kanisa, hija ya maisha ya imani, matumaini na m...

Kard. Parolin:ushuhuda wa mtakatifu rosalia sawa na watakatifu wengine wa sicilia - | vatican news

Katika maadhimisho ya Siku kuu ya miaka 400 ya heshima ya Mtakatifu Rosalia,msimamizi wa Kisiwa cha Italia,Katibu wa Vat...

Latests News

Israel,hali ya kibinadamu huko Gaza ni ya kukata tamaa.Maelfu ya watu wana njaa

Vita Nchi za Mashariki kati ya Israel na Palestina:vifo vingi kila siku.  (ANSA) Ulimwengu Israel,hali ya kibinadamu huk...

Monsinyo Wachowski; Atoa Tamko la kupinga nyanyaso za kijinsia!

Monsinyo Miroslaw S Wachowski, mwakilishi rasmi wa Vatican katika Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Mae...

Kard.Martínez Somalo alipenda Kanisa kwa akili na wema

Misa ya Maziko ya Kardinali Edoardo Martìnez iliyofanyika Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peto Vatican tarehe 13 agosti 2...

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Kazakhstan:picha na video za matukio ya kipapa

Katika siku yake ya mwisho  Alhamisi tarehe 15 Septemba 2022 Papa  atakutana na kuzungumza kwa faragha na Wayesuit wanao...

Dk. Ruffini:dira ya sinodi ni kanisa la kukaribisha wote - | vatican news

Ni kawaida kwetu kujiuliza:tuko wapi ulimwenguni,tuko wapi kwenye safari yetu?Tumefikia wapi? Na wapi?Na zaidi ya yote,j...

Top