Dk. Ruffini:dira ya sinodi ni kanisa la kukaribisha wote - | vatican news

Vaticannews

Dk. Ruffini:dira ya sinodi ni kanisa la kukaribisha wote - | vatican news"

Play all audios:

Loading...

Ni kawaida kwetu kujiuliza:tuko wapi ulimwenguni,tuko wapi kwenye safari yetu?Tumefikia wapi? Na wapi?Na zaidi ya yote,je,mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma,pamoja na


sehemu ndogo ya watu rahisi waliobatizwa ulisaidia?Ni maswali ya Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi. NA ANGELLA RWEZAULA, - VATICAN.


Kukutana pamoja, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikiliza kila mmoja kumesaidia kugundua tena kile kinachotuunganisha kuwa katika Kristo, kwa kutembea pamoja, ardhi


nzuri ambapo mbegu inaweza kukua; kushuhudia kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana; kuthamini daima, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe


kile kinachotutenganisha... Ndiyo maneno ambayo Dk. Paulo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi ambaye kila siku ya siku za


Sinodi akiwa amezungukwa na wasemaji aliweza kutoa habari ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea tangu kuanza kwa Sinodi ya XVI ya Maaskofu kuanzia tarehe 4 -29 Oktoba 2023, ikiongozwa na Mada


kuu:Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: USHIRIKA, USHIRIKI NA UTUME. Hata hivyo Sinodi hii imegawanyika katika awamu mbili ambapo ya kwanza imehitimishwa na ya pili ni Oktoba 2024. Mama baba


wa Sinodi na Mama   (Vatican Media) Kwa njia hiyo mara baada ya hitimisho la Sinodi hiyo, akitoa maoni yake katika Makala ya  Habari za Kikanisa SIR la Baraza la Maaskofu Italia kuhusiana na


tukio hilo muhimu, Dk Ruffini anabainisha kuwa  "baada ya kufikia hatua ya nusu ya Sinodi hii, ambayo inatutaka tujifikirie upya kama Kanisa, tunajikuta tukistaajabishwa katika


ulimwengu wenye mgawanyiko ambao "umepoteza njia ya amani, ambayo umempendelea Kaini kuliko Abeli" (Tazama Sala ya Papa Francisko ya amani ya 27.10.2023); sayari ambayo


"inabomoka na labda inakaribia mahali pa kuvunjika" (Papa Francisko, Laudate Deum,2). Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa hiyo anasisitiza kuwa "Ni kawaida kwetu


kujiuliza: tuko wapi ulimwenguni, tuko wapi kwenye safari yetu? Tumefikia wapi? Na wapi? Na zaidi ya yote, je, mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma ulisaidia, pamoja na


sehemu ndogo ya "watu rahisi waliobatizwa"? Je  ulisaidia nini? Washiriki wa Sinodi Akiendelea Dk Riffini anabainisha kuwa, “Hati ya muhtasari inaishia kwa kunukuu Injili ya Marko


(Mk 4.30 ) isemayo "Ufalme wa Mungu umefanana na mbegu ya haradali ambayo ikipandwa ardhini ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inakuwa kubwa sana hivi kwamba ndege wa angani wanaweza


kujificha kwenye kivuli chake. " Na hivyo  ndivyo ilivyokuwa kwa ajili ya kukusanyika, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikilizana kwa ajili ya kugundua tena kile


kinachotuunganisha kuwa katika Kristo; kutembea pamoja, ardhi nzuri ambapo mbegu inaweza kukua." Dk. Ruffini aidha anabainisha kwamba katika Sinodi hii ni wazi ilikuwa ni ushuhudia


kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana. Na hii ni kwa sababu lazima kuthamini kila wakati, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe kile


kinachotutenganisha. Kuelewa kwamba jukumu la ushirikiano ambalo kila mtu anaitwa, hata  katika utofauti wa karama na huduma ni huduma na sio nguvu. Vile vile ni kugundua upya  kwa jinsi


gani hotuba ya Yesu juu ya umaskini inatuhusu sisi sote, kama watu na kama taasisi. Zaidi pia ni kupendekeza na kuepuka ukasisi wowote (ule wa walei na ule wa mapadre waliowekwa wakfu).


Kujadili na kutembea pamoja   (Vatican Media) Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aidha alisisitiza kuwa ni kugundua tena umuhimu wa kila moja; na zaidi ya ushirika wote unaotufanya kuwa


wamoja, washiriki wa mtu mwingine. Kutafakari juu ya nafasi ya wanawake, ambao walikuwa wa kwanza kutangaza ufufuko wa Yesu. Kutoa msukumo mpya kwa uekumene. Kuwa Kanisa la kukaribisha watu


wote. Na zaidi kila mtu, ambapo hakuna mtu aliyetengwa. Kuwa Kanisa ambalo halifikirii kulingana na migawanyiko na alama za ulimwengu, lakini linalojiuliza kila wakati ikiwa Yesu angefanya


nini akikabiliwa na kaka au dada aliyejeruhiwa. Na ni kwa jinsi gani angehakikisha kutowatenga na ukombozi. Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi aidha alithibitisha jinsi ambavyo kuna changamoto


nyingi ambazo tunakabiliana nazo kama Kanisa. Zinahusu ukuhani, ushemasi, huduma zisizowekwa wakfu, maisha ya wakfu, familia na hali ngumu za ndoa; Huduma ya Kipetro, Uekumene, mawasiliano


katika enzi ya kidijitali. Pia zinahusu mada yenye utata wa utambulisho wa kijinsia na mwelekeo wa kijinsia. Kila siku Dr Ruffini na tume yake walihabarisha juu ya kinachoendelea cha Sinodi


  (Vatican Media) Dk. Ruffini alisisitiza kuwa, "lakini yote hayo ni upendo unaojumuisha wote. Sheria moja tu inaelezea Kanisa la Sinodi inayokubalika:ya  upendo; ubunifu wa


kimisionari wenye msingi mzuri, vumilivu, wema; “si lenye wivu, si lenye majivuno, si lenye kuvimba” (rej.1Kor 13:4). Hivi ndivyo Mkutano ulituambia ambao umehitimishwa hivi karibuni. Na


imetuonesha dira na siyo orodha ya mambo. Mamilioni, mabilioni ya watu ni kama msafiri aliyesafiri katika barabara kati ya Yerusalemu na Yeriko. Kwa hiyo hatuwezi kusema sikujua. Kwa hili


tutahukumiwa (rej. Mt 25).” Anahitimisha maoni yake Dk. Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi iliyaonza tarehe 4 hadi 29 Otoba


2023. Wakati wa kutoa taarifa ya sinodi   (Vatican Media) DK.Ruffini baada ya Sinodi


Trending News

Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 17:Wajumbe wanapendekeza marekebisho ya hati ya mwisho

Vatican Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 17:Wajumbe wanapendekeza marekebisho ya hati ya mwisho Katika mkutano wa waandishi w...

Idhaa ya kiswahili 16. 09. 2023 - | vatican news

__ The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the serv...

Sherehe Ya Huruma Ya Mungu: Yesu Ni Ufunuo Wa Huruma ya Mungu

UTANGULIZI: Dominika inayofuata baada ya Sherehe ya Pasaka ni Dominika ambayo Kanisa huadhimisha Sherehe ya Huruma ya Mu...

Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi Kongo

Mkuu wa timu ya kukabiliana na mpox nchini humo, Cris Kacita, ameonya kuwa kampeni ya kusambaza chanjo inaweza kuchukuwa...

Haiti:Zaidi ya nusu milioni ya watoto wako hatarini kwa magojwa ya mlipuko

Kwa mujibu wa tarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la  kuhudumia watoto, UNICEF linabainisha kuwa, watoto wapatao 540,0...

Latests News

Dk. Ruffini:dira ya sinodi ni kanisa la kukaribisha wote - | vatican news

Ni kawaida kwetu kujiuliza:tuko wapi ulimwenguni,tuko wapi kwenye safari yetu?Tumefikia wapi? Na wapi?Na zaidi ya yote,j...

Papa Francisko: utu na heshima ya binadamu vipewe kipaumbele katika tasnia ya habari!

Shirika la Habari la Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, SIR, linaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa...

Idhaa ya Kiswahili 30.08.2021 - | Vatican News

Podcast Idhaa ya Kiswahili 30.08.2021 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...

Sala kwa siku ya tatu ya babu, bibi na wazee duniani kwa mwaka 2023 - | vatican news

Siku ya Tatu ya Babu, Bibi na Wazee Duniani ni hapo Dominika tarehe 23 Julai 2023 kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Na rehem...

Papa Francisko: Utambulisho na vipaumbele katika utume wake!

Baba Mtakatifu Francisko kwa watu wengi duniani anaonekana kuwa ni chemchemi ya faraja na matumaini; mtetezi wa maskini ...

Top