Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili XIV: Utukufu wa Fumbo la Msalaba!

Vaticannews

Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili XIV: Utukufu wa Fumbo la Msalaba!"

Play all audios:

Loading...

Ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, karibu katika tafakari ya liturujia ya Neno la Mungu, dominika ya 14 ya mwaka C wa Kanisa, kipindi cha kawaida. Mama Kanisa katika dominika hii


anatukumbusha kuwa sisi sote tumeitwa kuihuburi Injili kwa kuishi Ukristo wetu vyema sio kwa sheria za maumbile bali kwa kuwa viumbe vipya ndani ya Kristo na kuona fahari juu ya Msalaba wa


Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwao tumekombolewa. Katika somo la kwanza kutoka sura ya mwisho ya kitabu cha nabii Isaya linatupa matumaini na faraja ya kushangilia na kufurahi kuwa Mungu


atasimamisha ufalme mpya wenye haki kwa wale wanaompenda na wanaomcha. Hii ni kusema kwamba wenye haki watashiriki baraka za milele katika mbingu mpya na nchi mpya yaani uzima wa milele.


Utabiri huu wa nabii Isaya unatimilika katika Kristo kwa kukombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mauti. Kazi imebaki kwetu kulisha na kuishi maisha ya kikristo. Wakati wa enzi za mitume


jumuiya zilizoipokea Injili zilikuwa na hamasa kubwa ziliikumbatia Imani. Furaha iliijaza mioyo yao. Walikuwa wachache kwa idadi, lakini waliishi imani hiyo kiaminifu na kwa furaha kubwa.


Furaha hiyo iliongezeka kadiri idadi yao ilivyoongezeka kwani wengi walipendezwa na maisha yao wakaamini na kubatizwa. Lakini taratibu, ile hamasa ilianza kufifia, ugomvi na mpasuko kati yao


ukaanza kutokea, wengi wakaanza kurudi nyuma katika imani yao. Wakristo katika Kanisa la Galatia nao walikata tamaa na kuanza kurudi nyuma katika imani. Katika mazingira hayo Paulo katika


somo la pili ambalo ni hitimisho la barua yake kali aliyowaandikia Wagalatia hata kuumbia, ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaloga? Akiwataka waujue ukweli na wasipotoshwe na mafundisho


ya uongo ya baadhi ya walimu wa uongo na Wayahudi wapotoshaji.


Mtume Paulo alikuwa amewahubiria watu wa Galatia katika safari yake ya kwanza ya kueneza Injili (Mdo 13:14-14:23). Baada ya yeye kuondoka, kikundi cha Wayahudi walioamini walifika, wakaanza


kusisitiza kwamba ni lazima watu wa Mataifa walioamini watimize kwanza sheria za Musa ili wapate kuokoka. Paulo anaandika kupinga mafundisho hayo kwa kuonyesha jinsi ambavyo Abrahamu, ambaye


aliishi miaka 400 kabla ya sheria ya Musa kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Anaonyesha kwamba, kama vile ambavyo sheria haiwezi kumwokoa mtu, hakuna mtu anayeweza kuwa mkamilifu kwa


kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe katika kutimiza sheria. Paulo anakazia hoja hiyo kwa kuthibitisha jinsi ambavyo yeye mwenyewe ni mtume wa Kristo na kwa kutoa mafundisho kuhusu jinsi


mkristo anavyopaswa kuishi. Paulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, Mtu anaokolewa kwa neema ya Mungu kwa kumwamini Kristo.


Mtu anayeongeza chochote katika ukweli huu anapotosha kweli ya Mungu. Tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya imani na tunakuwa watoto wa Mungu kwa imani. Kwa kuwa Kristo ametuweka


huru, basi tusimruhusu mtu yeyote aturudishe kwenye mawazo ya kudhania kuwa matendo ya sheria yanatosha kutupatia wokovu. Kama watu waliookolewa kwa neema, tuna wajibu wa kuishi maisha


yanayolingana na imani yetu. Ndiyo maana anasema, mimi hasha sioni fahari juu ya kitu cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa Yeye ulimwengu umesulibiwa kwangu,


nami nimesulibiwa kwa ulimwengu. Kwa maana katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu! Tangu sasa mtu ye yote asinitaabishe, kwa maana


nachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikae pamoja na roho zenu. Amina. Huu ni wosia wa Paulo kwa Kanisa la Galatia, ndio wosia kwetu sote tuliobatizwa


na kukubali kuwa Kristo ndiye mwokozi wa maisha yetu na kupigwa chapa ya Kristo ambayo ni msalaba.


Katika Injili Mwinjili Luka anasema, “Bwana aliweka wengine 72 nje na wanafunzi 12, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda katika kila mji alipokusudia kwenda mwenyewe. Namba 72


inasimama mahali pa makabila 72 au koo zilizoorodheshwa katika Sura ya 10 ya kitabu cha Mwanzo, namba kamili kama walivyofikiri Wayahudi, ikiwakilisha Makabila au Koo zote za dunia kwa


wakati ule. Huu ni ujumbe kuwa kutangaza habari njema ni jukumu la kila mmoja wetu. Hivyo kila mbatizwa anawajibu wa kumtangaza na kumshuhudia Kristo popote pale alipo katika maisha yake.


Wazazi wana jukumu la kuwaridhisha na kuwafundisha imani watoto wao. Watoto nao wanaowajibu wa kuwafundisha wazazi wao imani na kuwakumbusha wajibu wao katika maisha ya sala na kulitafakari


Neno la Mungu pale wanapojisahau. Mume anaalikwa kumpenda na kumwenjilisha mkewe, kadhalika mke anao wajibu kwa Mumewe kuona kwamba imani ndani ya familia inakuwa na kupewa kipaumbele


hususani kwa malezi na makuzi ya watoto.


Ndugu katika familia: Kaka, dada na marafiki wanapaswa kuhubiriana Habari Njema. Hivyo kila mwanafamilia ni Mmisionari kwa mwenzake. Kila mbatizwa ni mmisionari kwa mwenzake. Tukishirikiana


na maaskofu, mapadre, mashemasi na watawa tumpeleke Kristo katika maisha yetu ya kila siku. Tunapaswa kupeleka habari njema kwa wasio wakatoliki. Baadhi yao wakiwa ni ndugu zetu katika


familia: Siku hizi si ajabu ndani ya  kabila, ukoo  hata familia kuona kuna watu wa imani mbali mbali. Hivyo tunajukumu bado la kumshuhudia Kristo katika mazingira yetu ili watu wengine pia


wamjue. Kristo anatoa masharti katika kumtangulia akisema, “Msimwamkie mtu njiani” ili tusichelewe pia tusiweke matumaini yetu katika watu au vitu: “Msichukue mfuko wala fedha, wala viatu”.


Si fedha, wala elimu, wala mamlaka ya kibinadamu inayohitajika katika kumhubiri Kristo. Kinachohitajika ni ushuhuda wa maisha ya Kikristo na kuona fahari juu ya Msalaba.


Tunaitwa kuwa mabalozi wa amani na Upendo: ndiyo maana Kristo anasisitiza, katika kuenenda kwenu hii iwe ni salamu yenu: “Amani iwe ndani ya nyumba hii”. Kila Mkristo anapaswa kuwa mleta


amani na mpatanishi wakati wote. Hatuwezi kuwa waleta amani au wapatanishi ikiwa amani ya Kristo haimo ndani yetu. Tuombe daima imani hiyo na upendo wa Kristo utawale katika mioyo yetu na


katika jumuiya zetu. Tuwe jasiri na tusiokata tamaa katika kumshuhudia Kristo kwani anatuambia, “Na mji wowote mtakaoingia, nao hawakuwakaribisha, tokeni humo nanyi mkipita katika njia zake


semeni, hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandama na miguu yetu, tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili “Ufalme wa Mungu umekaribia”. Hatupaswi hata mara moja kukata tamaa, wala kuogopa.


Ukweli ni kwamba kuwaleta watu kwa Yesu kunaleta furaha kuu ndani ya mtu binafsi na katika Jumuiya. Wote wanaojitahidi kuwaweka watu huru kutoka utumwa wa shetani, wanapata nguvu


wanazohitaji katika shughuli hiyo ya kumshinda shetani. wakati wa majaribu kutoka kwa Mungu. Lakini furaha kubwa zaidi ni kuuridhi ufalme wa mbinguni ndivyo anavyotumbia Yesu: “Msifurahi kwa


vile pepo wamewatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”


Trending News

Idhaa ya kiswahili 25. 12. 2023 - | vatican news

__ The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the serv...

Idhaa ya kiswahili 15. 02. 2023 - | vatican news

__ The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the serv...

Hamas na fatah wakaribia makubaliano ya mtawala wa gaza

Afisa mmoja wa Mamlaka ya Palestina amethibitisha kwamba makubaliano ya awali yamefikiwa baada ya wiki kadhaa za mazungu...

Neema Singh Guliani

_Just Security_ is a non-profit, daily, digital law and policy journal that elevates the discourse on security, democrac...

Mama wa guadalupe:sala ya rosari takatifu katika uwanja wa mt. Petro - | vatican news

Tarehe 12 Desemba ni siku kuu ya Bikira Maria wa Guadalupe msimamizi wa bara la Amerika ya Kusini.Kabla ya Tafakari na s...

Latests News

Papa Francisko: Ujenzi wa Fumbo la Mwili wa Kristo: Sala na Ekaristi!

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kutoka kwenye Maktaba yake binafsi, Jumapili tarehe 15 M...

Marekani:ikiwa unataka amani fanya kazi kwa ajili ya haki! - | vatican news

Marais wa Tume ya Haki,amani na mandeleo fungamani,Tume ya wahamiaji na Tume ya kupinga ubaguzi wa rangi ya Baraza la Ma...

Sikukuu ya jina takatifu la yesu: maisha na utume wa yesu kristo - | vatican news

Jina Takatifu la Yesu linafafanua ndani mwake: Fumbo la Umwilisho linalopata hatima yake katika Fumbo la Pasaka yaani: M...

Papa francisko:upendo wa kristo unapitia katika ibada na matendo ya dhati - | vatican news

Baba Mtakatifu Francisko aliwaomba washiriki wa Kongamano la ‘Udugu na Ucha Mungu’ wa Watu huko Seville,Hispania,tarehe ...

Papa francisko apokea hati za utambulisho wa balozi wa australia - | vatican news

Balozi Chiara Porro alizaliwa tarehe 30 Julai 1984, ameolewa na kubahatika kupata zawadi ya watoto wawili. Ni msomi aliy...

Top