Barua ya mababa wa sinodi kwa vijana wote duniani! - | vatican news

Vaticannews

Barua ya mababa wa sinodi kwa vijana wote duniani! - | vatican news"

Play all audios:

Loading...

Mababa wa Sinodi kabla ya kufunga maadhimisho haya wamewaandikia vijana wote barua ambayo imesheheni: matumaini, imani na faraja kutoka kwao, ambao wamekuwa na fursa ya kusikiliza sauti ya


Kristo Yesu, ambaye ni kijana katika umilele wake. NA PADRE RICHARD A. MJIGWA, C.PP.S. – VATICAN. Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yaliyozinduliwa tarehe 3 Oktoba 2018


kwa kuongozwa na kauli mbiu “Vijana, Imani na Mang’amuzi ya Miito” yamefungwa rasmi, Jumapili tarehe 28 Oktoba 2018 kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye


Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Mababa wa Sinodi kabla ya kufunga maadhimisho haya wamewaandikia vijana wote barua ambayo imesheheni: matumaini, imani na faraja kutoka kwao,


ambao wamekuwa na fursa ya kusikiliza sauti ya Kristo Yesu, ambaye ni kijana katika umilele wake. Kwa njia ya Kristo, Mababa wa Sinodi wameweza kusikiliza sauti ya vijana, furaha yao,


malalamiko na ukimya wao. MABABA WA SINODI WANATAMBUA TAFAKARI ZA MAISHA YAO YA NDANI, FURAHA NA MATUMAINI; SHIDA NA MAHANGAIKO YANAYOWAKUMBA KATIKA SAFARI YA MAISHA YAO hapa duniani. Mababa


wa Sinodi wanawataka vijana kuwasikiliza, kwani wanapania kuwa ni washiriki wenza katika furaha ili matamanio yao halali yaweze kumwilishwa katika uhalisia wake. Kanisa ni Mama na mwalimu


kwa vijana, kumbe, hawezi kuwatelekeza kamwe, hadi pale matumaini yao yatakapotekelezwa. Mababa wa Sinodi wana uhakika kwamba, vijana wako tayari kujisadaka kwa njia ya maisha yao, ili ndoto


ya maisha iweze kumwilishwa katika uhalisia na katika historia ya binadamu! MABABA WA SINODI WANAKAZA KUSEMA, UDHAIFU, MAPUNGUFU YAO YA KIBINADAMU NA DHAMBI ZISIWE NI KIKWAZO KINACHOFIFISHA


IMANI. Kanisa ni Mama na kamwe hawezi kuwatelekeza, daima yuko tayari kuwasindikiza katika njia mpya, kwa kuwaongoza na kuwaelekeza mahali ambapo nguvu ya Roho Mtakatifu inataka kuwapeleka


kwa kuvunjilia mbali mawingu ya kutojali, ya kufanya mambo kwa juu juu tu pasi na kuzama katika undani wake na hatimaye, hali ya kukata tamaa! WAKATI AMBAPO MWENYEZI MUNGU ALIUPENDA


ULIMWENGU HATA AKAMTOA MWANAYE WA PEKEE, KRISTO YESU, UNAENDELEA KUTOPEA KATIKA: vitu, mafanikio ya haraka haraka, raha na starehe kwa kutumia migongo ya maskini; vijana wausaidie ulimwengu


kuweza kusimama tena na kuinua uso wake katika upendo, uzuri, ukweli na haki. Mababa wa Sinodi wanasema, kwa muda wa mwezi mzima, wametembea na baadhi ya vijana wenzao bila kusahau umati


mkubwa wa vijana uliowasindikiza kwa njia ya sala. MABABA WA SINODI WANATAMANI KUENDELEZA SAFARI HII KILA SEHEMU YA ULIMWENGU, PALE AMBAPO WANATUMWA NA KRISTO YESU KAMA WAFUASI WAMISIONARi.


Kanisa na ulimwengu katika ujumla wake, unahitaji ari na mwamko wa vijana. Wanawaalika vijana kuwa wanandani wa safari kwa vijana wenzao ambao ni dhaifu, maskini na wale ambao wamejeruhiwa


katika maisha. Vijana wawe ni mwanga angavu kwa sasa na kwa siku za usoni! Barua ya Maaskofu kwa Vijana


Trending News

George floyd: wamarekani weusi huwa katika hali gani kwenye mikono ya polisi? - bbc news swahili

GEORGE FLOYD: WAMAREKANI WEUSI HUWA KATIKA HALI GANI KWENYE MIKONO YA POLISI? Usomaji maandishi tu kupunguza gharama za ...

Kard. Re aongoza mazishi ya kardinali angelo amato:alikuwa mtu wa imani! - | vatican news

Dekano wa Makardinali aliongoza Ibada ya mazishi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican kwa ajili ya Kardinali Ama...

Papa francisko: ujenzi wa fumbo la mwili wa kristo: sala na ekaristi! - | vatican news

Umoja wa Fumbo la Mwili wa Kristo yaani Kanisa, unarutubishwa kwa njia ya sala na Fumbo la Ekaristi Takatifu hata kama k...

Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 - | Vatican News

Podcast Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...

Papa ameombea nchi pendwa ya myanmar ili vurugu ziishe - | vatican news

Papa Francisko amemwomba Mungu ili uchungu na vifo nchi Myanmar viishe na watu wasitoe machozi kamwe na mategemeo kuwa w...

Latests News

Barua ya mababa wa sinodi kwa vijana wote duniani! - | vatican news

Mababa wa Sinodi kabla ya kufunga maadhimisho haya wamewaandikia vijana wote barua ambayo imesheheni: matumaini, imani n...

Idhaa ya Kiswahili 15.01.2020 - | Vatican News

Podcast Idhaa ya Kiswahili 15.01.2020 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...

Mhutasari wa sinodi-siku ya 17:wajumbe wanapendekeza marekebisho ya hati ya mwisho - | vatican news

Katika mkutano wa waandishi wa habari wa Sinodi,wanajopo walijadili jukumu na mamlaka ya maaskofu,hitaji la sheria ya ka...

Majadiliano ya kiekumene ni sehemu ya vinasaba vya maisha na utume wa kanisa - | vatican news

Ni katika muktadha wa majadiliano ya kiekumene, Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 11 Julai 2024 jioni amekutana ...

Papa amemtua padre françois abeli muhoya mutchapa kuwa askofu wa kindu - | vatican news

Papa Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Kindu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)Mhesh.Padre François Abeli ...

Top