Paredi la ubingwa lasimamisha shughuli mjini leverkusen
Paredi la ubingwa lasimamisha shughuli mjini leverkusen"
Play all audios:
Maelfu ya mashabiki waliojawa na furaha walimiminika barabarani, huku baadhi yao wakifanikiwa kuligusa Kombe la DFB-pokal, walipoungana na vijana wa Xabi Alonso wakati wa msafara na
shamrashamra za kusherehekea ubingwa. "Binafsi, nimefarijika mno hasa baada ya kuwa shabiki wa Leverkusen tangu mwaka 1988 na kila wakati tukisubiri kushinda kombe. Na sasa, hatimaye
hilo limetokea. Tunajivunia," ameeleza mmoja wa mashabiki wa Leverkusen. Kilele za sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wao wa nyumbani Bay Arena. Soma pia: Alonso ahisi fahari na
uchungu baada ya 'Neverlusen' kushindwa Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso amesema, "Najivua sana kuwa na wachezaji na mashabiki hawa. Wajua, siamini kama msimu
umekamilika, msimu huu umekuwa kama ndoto. Hali imekuwa nzuri mpaka siku ya mwisho, ni kitu cha kufurahia, nguvu waliotupa mashabiki katika uwanja huu. Nafurahi sana kuwa na kikosi imara
kama hiki." Bayer Leverkusen ilimaliza msimu wa Bundesliga bila ya kupoteza mechi hata moja kwa kujikusanyia alama 90 na kumaliza alama 17 mbele ya Stuttgart iliyomaliza katika nafasi
ya pili na Bayern Munich, ambao ni mabingwa kwa misimu 11 iliyopita, ilitulia katika nafasi ya tatu.
Trending News
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA: Homa ya Mgunda, Ruangwa, Lindi - | Vatican NewsRais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, tarehe 12 Julai 2022 amepata fursa ya kuwahutubia wajumbe wa AMECEA, Jijini Dar es...
Safari ya Injili Ulimwenguni: Ushuhuda wa Mtakatifu Paulo!Mzunguko wa Katekesi kuhusu Safari ya Injili Ulimwenguni mintarafu Kitabu cha Matendo ya Mitume ni fursa ya kuendelea ku...
Idhaa ya Kiswahili 20.10.2023 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 20.10.2023 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Ethiopia:tumaini linaongezeka katika makubaliano ya amani huko Tigray - | Vatican NewsMsafara wa chakula kupelekwa huko Tigray ili kusaidia watu wanaoteseka na njaa. Kanisa Ethiopia:tumaini linaongezeka ka...
Idhaa ya Kiswahili 30.09.2022 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 30.09.2022 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Latests News
Paredi la ubingwa lasimamisha shughuli mjini leverkusenMaelfu ya mashabiki waliojawa na furaha walimiminika barabarani, huku baadhi yao wakifanikiwa kuligusa Kombe la DFB-poka...
Idhaa ya Kiswahili 20.10.2023 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 20.10.2023 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Ethiopia:tumaini linaongezeka katika makubaliano ya amani huko Tigray - | Vatican NewsMsafara wa chakula kupelekwa huko Tigray ili kusaidia watu wanaoteseka na njaa. Kanisa Ethiopia:tumaini linaongezeka ka...
Idhaa ya Kiswahili 30.09.2022 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 30.09.2022 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Papa:Mazungumzo kati ya watu wa dini tofauti ni kudumisha urafiki amani na maelewanoKila tarehe 16 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Stahamala au kuvumiliana iliyoanzishwa na Shirika la elimu,...