Ghana : mahama apata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi
Ghana : mahama apata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi"
Play all audios:
Tume ya uchaguzi ya Ghana bado haijatoa matokeo rasmi, lakini Mahamudu Bawumia, makamu wa Rais na mgombea wa chama tawala cha New Patriotic, alikiri kushindwa. Bawumia alitangaza kuwa
Waghana walitaka mabadiliko. _"Mabibi na mabwana, tumekubali kushindwa kama mwanademokrasia mkamilifu angefanya. Lakini hatujaachana na vita vya kubadilisha Ghana na kupanua fursa kwa
makundi yote ya jamii yetu. Hatutakuwa upinzani wa kuvuruga.", _ Kushindwa kwake kumemaliza miaka minane madarakani kwa chama cha NPP chini ya Rais Nana Akufo-Addo, ambaye muhula wake
wa mwisho ulikumbwa na msukosuko mbaya zaidi wa kiuchumi katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Kwa miaka mingi, Ghana ilishuhudia mfumuko mkubwa wa bei na kushindwa kulipa madeni. Mgombea
wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress, John Drahami Mahama, ametarajiwa kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi. Mahama aliwahi kuwa rais wa Ghana kutoka 2012 hadi 2017. Na
hili lilikuwa jaribio lake la tatu kugombea tena urais baada ya kushindwa katika chaguzi za 2016 na 2020. MATOKEO RASMI KUTANGAZWA JUMANNE Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jean Mensa baadaye
Jumapili alihimiza uvumilivu, baada ya mvutano kati ya vyama katika baadhi ya vituo ya kupigia kura kufuatia kucheleweshwa kutangaza matokeo. Hata hivyo vyama vya kisiasa vilikuwa na
mawakala wao katika vituo vya kupigia kura, ambao walichunguza na kujumlisha matokeo ya awali. Mahama bado hajazungumza hadharani. Lakini kwenye akaunti yake ya X, alithibitisha kupokea simu
ya pongezi kutoka kwa mgombea wa chama tawala kutokana na "ushindi wake mkubwa". Ubalozi wa Marekani mjini Accra pia ulipongeza huo ukiuita kuwa wenye mafanikio na unaoakisi
mapenzi ya watu wa Ghana. Marekani imeahidi kuendeleza ushirikiano wake wenye nguvu chini ya utawala wa rais mpya. UCHUMI MADA KUU YA KAMPENI Matatizo ya kiuchumi na mfumuko wa bei
vilighubika kampeni za uchaguzi, baada ya nchi hiyo, ya kwanza kutika uzalishaji dhahabu barani Afrika na mshafirishaji wa pili wa kakao duniani, kupitia mgogoro wa kushindwa kulipa madeni
na kuporomoka kwa thamani ya fedha, na kusababisha mkopo wa dola bilioni 3 kutoka kwa Shirika la Fedha Ulimwenguni, IMF. Hata hivyo, uchaguzi huo tulivu na wa amani umeonyesha ukomavu wa
demokrasia nchini Ghana.
Trending News
Tshisekedi: rwanda imepeleka raia wake maeneo ya m23Wakati wa hotuba yake mbele ya bunge, Rais Félix Tshisekedi alilaani mkakati unaodaiwa kuratibiwa na Rwanda wa kubadilis...
Vatican: usalama, utu na haki msingi za wakimbizi ni muhimu sana katika kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani. - | vatican newsBaba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume kama Khalifa wa Mtakatifu Petro anaendelea kutoa kipaumbele cha kwanza k...
George floyd: wamarekani weusi huwa katika hali gani kwenye mikono ya polisi? - bbc news swahiliGEORGE FLOYD: WAMAREKANI WEUSI HUWA KATIKA HALI GANI KWENYE MIKONO YA POLISI? Usomaji maandishi tu kupunguza gharama za ...
Kard. Re aongoza mazishi ya kardinali angelo amato:alikuwa mtu wa imani! - | vatican newsDekano wa Makardinali aliongoza Ibada ya mazishi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican kwa ajili ya Kardinali Ama...
Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Latests News
Macron, rais wa halmashauri kuu ya ulaya ziarani chinaWaliwasili mjini Beijing leo kwa ziara inayonuiwa kuishawishi China kutounga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, waka...
Idhaa ya Kiswahili 11.01.2019 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 11.01.2019 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
Mkutano wa rimini,balozi wa vatican huko kyiv:hapa ni ishara ya kutoa matumaini - | vatican news“Ikiwa unataka amani,tayarisha amani.”Ni maneno yaliyosemwa na Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas Balozi wa Vatican Nchini U...
Askofu emmanuel bushu wa jimbo la buèa ang'atuka kutoka madarakani - | vatican newsAskofu mstaafu Emmanuel Bushu wa Jimbo Katoliki Buéa alizaliwa tarehe 31 Julai 1944. Kumbe, ameng’atuka kutoka madarakan...
Kardinali parolin:kukarabatiwa kwa kambi itawezesha walinzi wa uswiss kutekeleza vema utume wao - | vatican newsKardinali Pietro Parolin amesema saini iliyotiwa Jumatano Mei 4 katika hati kwa ajili ya ukarabati wa kambi ya Walinzi w...