Papa:ikiwa tutajenga kwa pamoja ndugu wataona umoja - | vatican news
Papa:ikiwa tutajenga kwa pamoja ndugu wataona umoja - | vatican news"
Play all audios:
Papa Francisko akiadhimisha Misa kwa ajili ya Ufunguzi wa Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya katika kuadhimisha miaka 50 ya taasisi hiyo ameelekeza njia tatu za kupyaisha
ulaya:kutafakari,kujenga na kuona.Mungu ombi tujioneshe,lakini kuonesha Mungu kama walivyofanya Watakatifu.Hawana maneno,bali kwa ajili ya maisha. NA SR. ANGELA RWEZAULA – VATICAN. Papa
Francisko tarehe 23 Septemba 2021, wakati Mama Kanisa akiwa anakumbuka Mtakatifu Pio wa Pietralcina, ameadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro jioni saa 11.00 masaa ya
Ulaya kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya CCEE wakiwa katika kuadhimisha jubilei ya miaka 50 tangu taasisi hii izinduliwe. Papa Francisko
akianza mahubiri yake kuhusu masomo ya siku amesema kuwa: “Neno la Mungu leo hii linatupatia maneno matatu ya jinsi ambavyo tunapaswa wakristo na wachungaji Ulaya: KUTAFAKARI, KUJENGA na
KUONA. Akianza neno la kwanza ameseama KUTAFAKARI ni kile ambacho Bwana anatualika awali ya yote kufanya kwa njia ya nabii Hagai “fikirinei vizuri namna yenu ya mwenendo” na anarudia mara
mbili kwa watu wake (Hag, 1, 5.7).” Papa amesema “Je ni mantiki ipi ya mwenendo ambao walikuwa walitakiwa watafakari watu wa Mungu?. Bwana anawambia “Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika
nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?(Hag 1,4). Watu walio kuwa wametoka utumwani walikuwa wanahangaikia kujali makazi yao. Kwa maana hiyo sasa
wanafurahia kukaa vizuri na utulivu nyumbani wakati Hekalu la Bwana ni magofu na hakuna anayekarabati. Huo ni mwaliko wa kutaka utafakari, kwa maana hata leo hii katika Ulaya, sisi wakristo
tuna vishawishi vya kukaa vizuri katika miundo yetu, nyumba zetu na makanisa yetu, katika usalama ambao ulitokana na tamaduni ziliolipa gharama kwa namna fulani, wakati mahekalu yanayo
tuzungua yanakuwa matupu na Yesu anaendelea kusahauliwa, Papa amesema. [embedded content] Misa ya Papa na Maaskofu wa CCEE Misa kwa ajili ya Maaskofu wa CCEE Kwa maana hiyo kutafakari, watu
hawa hawana tena njaa na kiu ya Mungu! Si kwamba ni wakatili hapana, lakini ni kwa sababu wanakosa anayewafanya wawe na njaa ya imani, na kuwaacha tena hiyo kiu iliyofifia na ya kudumu
ambayo Dante anazungumza (Paradiso, II, 19) na ambayo udikteta wa utumiaji, udikteta mwepesi lakini unaokosesha nguvu, unajaribu kuzima. Wengi wanaongozwa kuhisi mahitaji ya kiulimwengu
tu, sio ya ukosefu wa Mungu. Na hakika tuna wasiwasi juu yake, lakini ni kiasi gani tunajali juu yake? Ni rahisi kuwahukumu wale ambao hawaamini, ni rahisi kuorodhesha sababu za ubashiri,
uaminifu na mambo mengine mengi lakini mwishowe ni tasa. Neno la Mungu linatuongoza kutafakari juu yetu wenyewe: Je! Tunahisi mapenzi na huruma kwa wale ambao hawajapata furaha ya kukutana
na Yesu au wamepotea? Je! Tumetulia kwa sababu kimsingi hatukosi chochote cha kuishi, au tuna wasiwasi kuona kaka na dada wengi wako mbali na furaha ya Yesu? Misa kwa ajili ya Maaskofu wa
CCEE Katika jambo jingine, Bwana kwa njia ya Nabii Hagai, anawaomba watu watafakari nia zao na kusema “Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini
hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto ( Hag 1,6). Kwa namna hii watu walikuwa na kila walichotaka lakini hawakuwa na furaha. Je walikosa nini? Yesu mwenyewe
anashauri kupitia maneno ambayo ni kama yake ya Hagai “Nilikuwa na njaa hamkuja kunipatia chakula, nilikuwa na kiu hamkunipa cha kunywa(…) nilikuwa uchi, hamkunivalisha nguo (Mt 25, 42-43).
Ukosefu wa upendo husababisha kutokuwa na furaha, kwa sababu ni mapendo tu yanaridhisha moyo. Upendo tu huuridhisha moyo. Kufungwa ndani ya masilahi ya vitu vyao wenyewe, wenyeji wa
Yerusalemu walikuwa wamepoteza ladha ya ukarimu. Inaweza pia kuwa shida yetu: kuzingatia nyadhifa mbali mbali Kanisani, kwenye mijadala, ajenda na mikakati, na kupoteza mtazamo wa mpango
halisi, wa Injili: msukumo wa upendo, shauku ya ukarimu. Njia ya kutoka kwa shida na kufungwa daima ni ile ya zawadi ya bure. Hakuna nyingine, Papa amesisitizia hilo mara tatu! kwa maana
hiyo Papa ameomba kutafakari. Misa kwa ajili ya Maaskofu wa CCEE Baada ya kutafakari kuna hatua ya pili, ambayo ni kukrabati. Kwa njia ya nabii anawambia “mnijengee nyumba” (Hag 1,8). Watu
wlaijenga nyumba. Waliacha kufurahia waliyokuwa nayo na kufanya kazi kwa ajili ya wakati ujao. Katika hili ndicho kinahitajika kujenga nyumba ya pamoja ya Ulaya. Kuacha urahisi wa haraka
ili kurudi katika maono ya muda mefu ya Mababa waanzilishi, maono ya kinabii na ya pamoja kwa sababu hayatafuti maana ya wakati uliopo tu, lakini walikuwa wakiota ya wakati ujao kwa ajili ya
wote. Kwa maana hiyo walijenga kuta za nyumba ya Ulaya na ndiyo hiyo tu inaweza kuwa thabiti. Hii inahitajika hata kwa Kanisa, nyumba ya Mungu. Ili iweze kuwa nzuri na karimu, inahitajika
kutazama pamoja wakati ujao na siyo kukarabati wakati uliopita. Kwa kila mtu kuanzia na misingi hii kwani ndiyo panajengeka: kutoka katika tamaduni hai za Kanisa ambazo zimejikita kwenye
misingi muhimu, juu ya tangazo jema, juu ya ukaribu na juu ya ushuhuda. Kuanzia hapo ndipo panajenga, misingi ya Kanisa ya asili na ya daima, kuabudu Mungu na kutoka katika upendo wa jirani
na siyo kwa ajili ya matakwa maalum binafsi. Maadhimisho ya misa Takatifu kwa ajili ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE) Papa Francisko akiendelea na mahubiri, kwa maana hiyo amependa kuwashukuru
kwa kazi hiyo ambayo si rahisi ya ujenzi ambao wanapeleka mbele kwa neema ya Mungu. Anawashukuru kwa miaka hii 50 ya kwanza ya huduma ya Kanisa na Ulaya. Anasema watiwe moyo bila kukata tama
na kujiachia, kwa maana wameitwa na Bwana katika kazi nzuri angavu, kufanya kazi ili nyumba yake iwe daima ya makaribisho zaidi , kwa sababa kila mmoja aweza kuingia na kukaa, kwa sababu
Kanisa liweze kuwa mlango wa wote na hakuna kishawishi cha tazama tu na kubadilisha kitasa. Watu wa Israeli walijenga hekalu kwa mikono yao. Wajenzi wakuu wa imani wa Bara la Ulaya walifanya
hivyo hivyo. Walithubutu udogo wao, kwa kumwamini Mungu. Papa amefikiria kama Mtakatifu Martino, Francis, Dominiko, Pio ambaye amekumbukwa leo hii: wasimamizi wa Ulaya kama Benedikto,
Cirilly na Methodius, Brigita, Katarina wa Siena, Teresa Benedetta wa Msalaba. Hawa amesema walianzia kubadilisha maisha yao binafsi kwa kupokea neema ya Mungu. Hawakuangaika kwa sababu ya
nyakati za giza, mikanganyo na migawanyiko kadhaa, ambayo imekuwapo daima. Misa kwa ajili ya Maaskofu wa CCEE Hawakupoteza wakati wowote kukosoa na kulaumu. Waliishi injili, bila kujali
umuhimu na siasa. Kwa njia hiyo ya nguvu ya unyenyekevu wa upendo wa Mungu, waliweza kuingia katika mtindo wake wa ukaribu, huruma na upole ambao ndiyo kweli wa Mungu, na walijenga
monasteri, walitoa ardhi, na kuhuisha roho watu na Nchi, na kwa maana hiyo hakukuwa na mpango wa kijamii bali Injili. Jengeni nyumba yangu. Ni neno la kuunganisha kwa pamoja. Kila ujenzi
unafanyika kwa pamoja, katika ishara ya umoja, Papa amebainisha. Na wengine. Inawezekana kuwapo maoni tofauti, lakini daima yanalinda umoja. Kwa sababu ikiwa tunalinda neema ya pamoja,
Bwana anajenga hata pale ambapo hatuwezi. Ni wito wetu wa kuwa Kanisa, Mwili mmoja kati yetu. Ni wito wetu kama Wachungaji kukusanya zizi na siyo kulipoteza na wala kulihifadhi katika zizi
zuri lililofungwa. Kujenga tena maana yake ni kuwa fundi wa mungano , msukaji wa umoja kwa kila ngazi, si katika mkakati lakini Injili. Ikiwa tunajenga, tutawapatia uwezekano kaka na dada
zetu KUONA. Papa amesema Neno la tatu ambalo linahitimishwa katika Injili ya siku na Erode, ni ambaye alikuwa anataka kuona Yesu (Lk 9,9). Leo hii kama hapo awali wanazungumzia sana juu ya
Yesu. Katika wakati ule walikuwa wanasema “Yohane amefufuka katika wafu (…) Alimtokea Elia (…) Alifufuka mmoja wa manabii (Lk 9,7-8). Wote hao walikuwa wanamsifu Yesu, lakini hawakuelewa
mapya yake, walikuwa WAKIMFUNGIA katika muundo wa kile ambacho wamekwisha ona: Yohane, Elia na manabii… Yesu lakini hawezi kumfungiwa katika muundo wa “kusikia ‘wanasema ’ au ‘nilisha ona.’
Wengi katika Ulaya wanafikiria kuwa imani ni jambo ambalo limekwisha onekana, ambalo ni la kizamani, Kwanini? Kwa sababu hawakuona Yesu katika matendo yao katika maisha. Na mara nyingi
awakuona kwa sababu sisi katika maisha yetu hatumuoneshi vya kutosha. Kwa sababu Mungu anaonekana katika sura na katika ishara za wanaume na wanawake waliobadilishwa na uwepo wake. Misa
kwa ajili ya Maaskofu wa CCEE Ikiwa Wakristo badala ya kuwa na furaha iliyotokana na Injili, wanapendekeza muundo wa kidini mbaya, wa wasomi na wamaadili, watu hawaoni mchungaji Mwema.
Hawajuhi Yule ambaye anampenda kila kondoo, anamwita kwa jina na kumtafuta ili amweke mabegani, Yeye ana huruma tu kwa ajili ya mtu. Upendo huo, na huruma hiyo ni ya kushangaza, ni mapya ya
daima ya Injili. Swali linalokuja kwetu sisi tuliochaguliwa na shauku, Papa amesema “fanyeni kwa niaba ya upole wa ajabu ambao Kristo alituokoa. Hatuombi tujioneshe, lakini kuonesha Mungu
kama walivyofanya Watakatifu. Hawakuwa na maneno, bali kwa ajili ya maisha. Anaomba sala na umaskini, anaomba ubunifu na kujitoa bure. Tusaidie Ulaya ya leo iliyougua na uchovu ili iweze
kupata sura ya kijana daima ya Yesu na Mchumba wake. Hatuwezi kutoacha kujitoa sisi wenyewe ili uzuri huu usioisha uweze kwenda mbele”.
Trending News
Vatican: usalama, utu na haki msingi za wakimbizi ni muhimu sana katika kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani. - | vatican newsBaba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume kama Khalifa wa Mtakatifu Petro anaendelea kutoa kipaumbele cha kwanza k...
George floyd: wamarekani weusi huwa katika hali gani kwenye mikono ya polisi? - bbc news swahiliGEORGE FLOYD: WAMAREKANI WEUSI HUWA KATIKA HALI GANI KWENYE MIKONO YA POLISI? Usomaji maandishi tu kupunguza gharama za ...
Kard. Re aongoza mazishi ya kardinali angelo amato:alikuwa mtu wa imani! - | vatican newsDekano wa Makardinali aliongoza Ibada ya mazishi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican kwa ajili ya Kardinali Ama...
Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 - | Vatican NewsPodcast Idhaa ya Kiswahili 25.12.2023 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...
404 - ukurasa haujapatikanaNenda kwenye maudhuiNenda kwenye orodha kuuNenda tovuti zaidi za DWVidio zetuSauti zetuMaeneoTanzaniaKenyaJamhuri ya Kid...
Latests News
Papa:ikiwa tutajenga kwa pamoja ndugu wataona umoja - | vatican newsPapa Francisko akiadhimisha Misa kwa ajili ya Ufunguzi wa Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya katika kua...
YAKISUGI cajon | designboom.comDESIGNER'S OWN WORDS:着火剤としても使用される燃えやすい杉材を建築に使おうとする1つの矛盾を、「焼けないように焼いておく」という発想で解決した先人の知恵を、今回のテーマを見たときに思い出しました。焼杉は日本の伝...
Papa Francisko:Teknolojia zijali kwanza kiini cha mwanadamu2024.02.12 Papa alikutana na wajumbe washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Chuo cha Kipapa cha Maisha, (Vatican Media...
Kard.Parolin kwa G20:Mataifa ya baada ya Vita ya II ya Dunia zina changamoto kujibu madai ya karne ya 21Hotuba ya Kardinali Pietro Parolin katika G20 - tarehe 18 Novemba 2024. Vatican Kard.Parolin kwa G20:Mataifa ya baada y...
Hija ya Papa Francisko nchini Morocco: Mhudumu wa matumainiMtakatifu Yohane Paulo II kwa mara ya kwanza katika historia, alitembelea nchini Morocco kunako mwaka 1985 wakati wa maa...