Tanzia: kardinali josé freire falcão oktoba 1923 - sept. 2021 - | vatican news

Vaticannews

Tanzia: kardinali josé freire falcão oktoba 1923 - sept. 2021 - | vatican news"

Play all audios:

Loading...

Kardinali José Freire Falcão, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Brasilia nchini Brazil amefariki dunia kwa Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 hapo tarehe 26 Septemba 2021, akiwa na


umri wa miaka 95. Mazishi yake yamefanyika tarehe 27 Septemba 2021 kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria waAparecida, Jimbo kuu la Brasilia. Ni kiongozi aliyejipambanua kwa karama na utume! NA


PADRE RICHARD A. MJIGWA, C.PP.S. –VATICAN. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa za kifo cha Kardinali José Freire Falcão, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Brasilia


nchini Brazil aliyefariki dunia kwa Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 hapo tarehe 26 Septemba 2021, akiwa na umri wa miaka 95. Mazishi yake yamefanyika tarehe 27 Septemba 2021 kwenye


Kanisa kuu la Bikira Maria waAparecida, Jimbo kuu la Brasilia. Kardinali José Freire Falcão tarehe17 Septemba 2021 alilazwa kwenye Hospitali ya Santa Lúcia, Jimbo kuu la Brasília na hali


yake ikaendelea kuwa mbaya siku kwa siku. Baba Mtakatifu katika salam zake za rambirambi alizomwandikia Askofu mkuu Paulo Cezar Costa wa Jimbo kuu la Brasilia, anasema, anapenda kuungana na


familia ya Mungu Jimbo kuu la Brasilia kuomboleza kifo cha Kardinali José Freire Falcão na kwamba, anamwaminisha kwenye huruma ya Mungu, akikumbuka mchango wake mkubwa katika ustawi,


maendeleo na mafao ya Kanisa katika ujumla wake. NI KIONGOZI ALIYEKUWA NA ARI NA MWAMKO WA UINJILISHAJI, DAIMA ALIPENDA KUKUTANA NA WAAMINI WAKE. Alionesha mapaji aliyokirimiwa na Mwenyezi


Mungu hasa wakati alipokuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Brazil. Baba Mtakatifu anapenda kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shurani kwa huduma yake makini ya: kufundisha,


kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kama Askofu. Ni kiongozi aliyejisadaka bila ya kujibakiza, akaonesha ukarimu mkubwa kwa watu wa Mungu, huku akiwaongoza katika njia ya kweli za


Kiinjili, kama alivyokuwa anatekeleza dhamana na wajibu wake hata kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu. Baba Mtakatifu anapenda kumweka Hayati Kardinali José Freire Falcão, Askofu mkuu mstaafu wa


Jimbo kuu la Brasilia chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria pamoja na watu wote wa Mungu Jimbo Katoliki la Brasilia. Baba Mtakatifu ametoa baraka zake za kitume kwa wale wote walioshiriki


mazishi ya Kardinali José Freire Falcão, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Brasilia nchini Brazil. ITAKUMBUKWA KWAMBA, HAYATI KARDINALI JOSÉ FREIRE FALCÃO, ASKOFU MKUU MSTAAFU WA JIMBO


KUU LA BRASILIA ALIZALIWA TAREHE 23 OKTOBA 1923 HUKO ERERE NCHINI BRAZIL. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 19 Juni 1949 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baada ya miaka


18 ya Upadre, tarehe 24 Aprili 1967 akateuliwa kuwa Askofu mwandamizi wenye haki ya kurithi Jimbo la Limoeiro do Norte na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 17 Juni 1967. Tarehe 25 Novemba 1971


akateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Teresina na kuliongoza kwa takribani miaka 12. Tarehe 15 Februari 1984 Mtakatifu Yohane Paulo II akamwamishia Jimbo kuu la Brasilia ambako


ameliongoza kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20. Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa ni Kardinali tarehe 28 Juni 1988. Ni kiongozi wa Kanisa aliyejisadaka kwa ajili ya ustawi, maendeleo


na mafai ya watu wa Mungu katika ujumla wao. Alisimama kidete kutangaza na kushuhudia ukweli na tunu msingi za Kiinjili. Alilipenda Kanisa na watu wake kutoka katika sakafu ya maisha yake.


Aling’atuka kutoka madarakani tarehe 28 Januari 2004. Amefariki dunia akiwa amewafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa miaka 72 kama Padre, Miaka 54 kama Askofu na miaka


33 kama Kardinali. Kutokana na kifo chake, kwa sasa kuna Makardinali 217 na kati yao kuna Makardinali 121 ambao wanaweza kupiga au kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu


Petro. Tanzia Brasilia


Trending News

Bolsas da europa fecham em forte alta

As principais bolsas da Europa fecharam em alta nesta sexta-feira, animadas por resultados corporativos positivos, pela ...

Exportação de carne só se normaliza em seis meses

O resultado negativo dos exames realizados pelo Laboratório Nacional Agropecuário (Lanagro), que descarta a existência d...

Dilma: denúncias do senador delcídio são levianas e mentirosas

A presidente Dilma Rousseff disse nesta quarta-feira (4) que as denúncias feitas pelo senador Delcídio do Amaral (sem pa...

Deputados cobram do governo envio de cálculos sobre a previdência

09/03/2017 07h15 DEPUTADOS COBRAM DO GOVERNO ENVIO DE CÁLCULOS SOBRE A PREVIDÊNCIA O secretário da Previdência do Minist...

Eleições 2024: veja a lista dos vereadores eleitos em extrema - mg

EXTREMA conheceu neste domingo, 6 de outubro, seus mais novos 13 vereadores, após a conclusão da contagem de votos do 1º...

Latests News

Tanzia: kardinali josé freire falcão oktoba 1923 - sept. 2021 - | vatican news

Kardinali José Freire Falcão, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Brasilia nchini Brazil amefariki dunia kwa Ugonjwa wa ...

Desempenho

ExploreSexta-feira, 13 de Junho de 2025ENTRAREncontre matérias e conteúdos da Gazeta doPovoNotíciasSaberÚltimasEditoriai...

Libertadores: flamengo aparece como principal favorito ao título da competição continental | coluna do fla

_Apesar de críticas por conta do desempenho, Fla surge como principal candidato a levantar o troféu em 2022_ O Flamengo ...

Dia mundial sem carne é comemorado nesta segunda-feira

_NO BRASIL, PESQUISAS APONTAM QUE POPULAÇÃO TEM O DESEJO CADA VEZ MAIOR DE REDUZIR O CONSUMO DE PROTEÍNA ANIMAL_ Nesta s...

Flamengo contrata ex-diretor do vasco para as finanças. | coluna do fla

Extra Globo – Ex-diretor-geral do Vasco, o executivo Cristiano Koehler, está sendo contratado pelo Flamengo como consult...

Top