Gaza, ukraine, sera ya ndani vyatia kiwingu urathi wa biden

Dw

Gaza, ukraine, sera ya ndani vyatia kiwingu urathi wa biden"

Play all audios:

Loading...

Akiwa amesalia na mwezi mmoja tu madarakani, Biden anakabiliana na orodha ndefu ya hatua za sera za ndani na njeanazotaka kukamilisha kabla ya Rais mteule Donald Trump kuingia ofisini,


ambapo inatarajiwa kuwa Trump atajaribu kubatilisha mafanikio mengi ya Biden. Miongoni mwa vipaumbele vya Biden ni kushinikiza usitishaji wa mapigano Gaza, kuachiliwa kwa mateka wa Marekani


nje ya nchi, kupeleka msaada zaidi kwa Ukraine, kutoa msamaha kwa wafungwa wasio na hatia ya vurugu, na kusamehe madeni zaidi ya wanafunzi. Aidha, anapanga kutoa ufadhili zaidi kwa


uzalishaji wa chipu za semiconductor zinazotumika kwenye vifaa karibu vyote mambeleo vya mawasiliano . Vilevile, Biden anatazamiwa kuzuia uwezekano wa kuuzwa kwa kampuni ya chuma ya


Marekani, kabla ya kuondoka madarakani, hatua zinazolenga kuimarisha urathi wake na kuhakikisha baadhi ya mipango yake inasalia hata baada ya Trump kushika hatamu. Orodha hiyo inaonyesha


jinsi vita vya muda mrefu na vya umwagaji damu barani Ulaya na Mashariki ya Kati wakati wa uongozi wa Biden vilivyoharibu urathi wake wa kimataifa, ambapo aliahidi kurejesha na kuimarisha


uongozi wa Marekani. Wakati huohuo, kushindwa kwa Democrats katika uchaguzi kumeitikisa historia yake ya kisiasa nyumbani. Soma pia: Biden amkaribisha Trump Ikulu ya White House Biden,


mwenye umri wa miaka 82, aliahidi kubadilisha uchumi wa Marekani akiwa rais na alipata mafanikio makubwa ya kisheria katika nusu ya kwanza ya muhula wake wa miaka minne, ikiwa ni pamoja na


miswada ya miundombinu iliyoungwa mkono na vyama vyote, na kupunguza mfumuko wa bei. Hata hivyo, utungaji mkubwa wa sheria ulisimama kabisa baada ya Warepublican kuchukuwa udhibiti wa Bunge


la Wawakilishi katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022. Baadhi ya Wademorat wanamlaumu Biden kwa kukataa awali kujiondoa kama mgombea, hatua ambayo wanadai ilisababisha kushindwa kwao


vibaya mwezi Novemba, hasa Makamu wa Rais Kamala Harris kushindwa na Trump katika kila jimbo muhimu la uchaguzi. TRUMP: USHINDI HUU NI MAGEUZI MAKUBWA YA KISIASA To view this video please


enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video VIPAUMBELE VYA BIDEN Kuhakikisha mpango wa kusitisha vita kati ya Israel na Hamas, ambamo mamlaka ya


Wapalestina inasema zaidi ya watu 45,000 wameuawa Gaza, na kuimarisha ulinzi wa Ukraine katika vita vyake vya karibu miaka mitatu na Urusi ni vipaumbele vya juu, kwa mujibu wa maafisa wa


Ikulu ya Marekani. Mwanahistoria wa marais wa Marekani na profesa wa Chuo Kikuu cha Vanderbilt, Thomas Alan Schwartz, anasema si jambo la kawaida kwa marais mwishoni mwa muhula wao au katika


kipindi cha mpito kukabiliana na migogoro ambayo haijatatuliwa. Soma pia: Trump afanya uteuzi mpya, Rubio anatazamiwa kuwa waziri wa mambo ya nje Mpango wa kusitisha mapigano katika vita


vya miezi 14 Gaza unaweza kufikiwa katika siku chache zijazo, huku serikali ikifanya juhudi kubwa za kidiplomasia wiki hii. Majadiliano kama hayo yenye matumaini yamewahi kuvunjika hapo


awali, lakini makubaliano haya yana lengo finyu zaidi. Biden anaharakisha kuisaidia kwa silaha Ukraine kwa hofu kwamba Trump anaweza kukata msaada kabisaa, huku akijaribu kufikia makubaliano


ya usalama na Saudi Arabia, licha ya kukataa kwa taifa hilo kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel. Biden anatarajiwa kuzuia uuzaji wa kampuni ya chuma ya Marekani kwa mnunuzi wa nje wiki


ijayo, akitimiza ahadi yake ya kulinda viwanda vya ndani. Kamati ya uwekezaji wa nje ya bunge, CFIUS, ina hadi Desemba 23 kuidhinisha au kukwamisha mpango huo, jambo ambalo hata Trump


alisema angefanya. Soma pia: Je, ni kwa kiasi gani Warepublican wanaweza kubadilisha Marekani? Hata hivyo, Biden anakimbizana kutekeleza sera nyingine kama kupunguza athari za mabadiliko ya


tabianchi, ambazo Trump anapinga. Wizara za Fedha na Biashara pia zinakamilisha miradi muhimu, ikiwemo uzalishaji wa chip, huku mustakabali wake ukibaki mashakani chini ya Trump. Chanzo:


Reuters


Trending News

Raia | designboom.com

DESIGNER'S OWN WORDS: RAIA brings the feeling of freedom to the user by allowing a great variety of position adjust...

Papa Francisko:Teknolojia zijali kwanza kiini cha mwanadamu

2024.02.12 Papa alikutana na wajumbe washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Chuo cha Kipapa cha Maisha,   (Vatican Media...

Papa francisko maskini ni amana, utajiri na walengwa wa uinjilishaji - | vatican news

Papa Francisko ametuma ujumbe wa video kwa wafanyakazi wa kujitolea wa “Huduma ya Upendo wa Usiku pamoja na Nyumba ya Na...

Kishengaga

Kashmir Will repatriate body of PaK minor fished out from Kishengaga river: Police Bymigrator July 10, 2019 No Comments ...

Papa:wayahudi na wakristo wanaokiri muumba mmoja wanaweza kufungua njia za amani! - | vatican news

Katika mkutano na wawakilishi wa Jukwaa la Kimataifa la Kiyahudi,Papa Francisko amebainisha kwamba kila vita siku zote,k...

Latests News

Gaza, ukraine, sera ya ndani vyatia kiwingu urathi wa biden

Akiwa amesalia na mwezi mmoja tu madarakani, Biden anakabiliana na orodha ndefu ya hatua za sera za ndani na njeanazotak...

Maadhimisho ya siku ya vijana duniani 2023: msalaba wa vijana! - | vatican news

Baraza la Maaskofu Katoliki Ureno linapenda kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu kabla na wakati wa Maadhimisho ya ...

Mchango wa mababa wa kanisa kuhusu: utu na uhuru wa kidini! - | vatican news

Mtakatifu Paulo VI alichangia katika maboreho na hatimaye tamko kuhusu Uhuru wa Kidini kwani hakuna mtu anayepaswa kuzui...

Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 06 Januari 2020 - | Vatican News

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Bwana awe nanyi ! Awe rohoni mwa...

Idhaa ya Kiswahili 14.07.2020 - | Vatican News

Podcast Idhaa ya Kiswahili 14.07.2020 Your browser does not support the audio element Mchango wako kwa ajili ya utume mp...

Top